15 Novemba 2014 - 15:31
Balaa liliosababishwa na Daesh nchini Tunisia

Idadi ya wananchi wengi wa nchini Tunis walio athiriwa na fikra za kigaidi za daesh inaendelea kuzidi nchini humo kiasi kwamba inadhaniwa kufikia kati ya elfu 10 au elfu 15 katika nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vikundi vya kigaidi nchini Tunis katika mwaka mmoja nchini humo vimefanya vitendo vingi vya kigaidi nchini Tunis, hii ni katika hali ambayo nchi hiyo na nchi nyingine jirani imekuwa ndio makimbilio ya kuchukua nguvu mpya ya msaada kwa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria na Iraq.
Kitendo cha kigaidi cha mwisho nchini humo kimefanyika wiki iliopita ambapo magaidi wanao fungamano na kikundi cha kigaidi cha Daesh walivamia gari la jeshi la Tunis katika mipaka ya nchi hiyo na Algeria na kuuwa wanajeshi wa tano wa Tunisia.
Idadi ya wananchi wa Tunisia ambao wameathiriwa na fikra za kigaidi za Daesh imezidi na kufikia idadi kubwa ambapo baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa ni baina ya watu elfu 10 au 15 elfu waliopo nchini humo.
Serikali ya Tunis baada ya tukio hilo imetangaza rasmi kuwa mwananchi yeyote anayejihusisha na fikra za kikundi hicho cha kigaidi bila shaka imewekwa adhabu kali kwa mwananchi atakaye jihusisha na masuala hayo, katika hali hiyo pia waziri mkuu wa Tunis ametoa taarifa kuwa serikali ya Tunis imezuia safari za vijana elfu 9 waliokuwa wakitaka kusafiri kuelekea nchini Syria na Iraq kuungana na vikundi vya kigaidi vya Daesh katika nchi hizo.
Wizara hiyo imetoa ripoti rasmi ya idadi ya Watunis walioko nchini Iraq na Syria kuwa ni watu 2500, katika hali ambayo ripoti za umoja wa mataifa zinaeleza kuwa idadi ya magaidi waliotoka nchini Tunisia waliopo nchini Iraq na Syria kuwa ni watu 3000 ambayo ni asilimia 80 ya wanajeshi wote wa Daesh katika nchi hizo.
Vyombo vya ulinzi vya nchi hiyo vimetangaza kuwepo wanachama wa Daesh 420 katika nchini hiyo ambapo makazi yao yako katika mikoa 13 ya nchi hiyo. hii ndio hali nzito ilioipata taifa hilo ambalo lilikuwa likiwahami magaidi hao wadaesh na sasa kugeuka kuwa tishio dhidi ya taifa hilo.